Eneo la Neema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waebrania 4:16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Je!, Unaweza kukumbuka ulipokuwa kijana jinsi kipindi kile kilivyokuwa kigumu. Ulikuwa kama mtoto lakini unachanganya kila kitu, karibu kila mtu alikuwa hakuelewi.
kweli ni hali mbaya sana pale watu wanapokuwa hawakuelewi. Wewe ni wewe, unaangalia mambo kwa kutumia macho yako mawili na kujisikia kulingana na hisia zako za ndani … lakini, hakuna hata mtu mmoja anakuelewa! Unaweza kuzungukwa na umati mkubwa wa watu wenye nia njema, lakini bado unajisikia kuwa mpweke.
Ndivyo wanavyojisikia wengine pale wewe na mimi tunaposhindwa kuwaelewa; pale tunapowahukumu watu kwa haraka, kabla hatujajaribu kutembea maili moja tukiwa tumevaa viatu vyao ili tuelewe vizuri kinachoendelea ndani ya mawazo yao.
Jana tulisimulia habari za Mungu kwamba hata kama anajua kila kitu wakati wo wote, bado aliamua kufanyika mtu aitwaye Yesu na kujaribiwa kwa njia zote kuwa kama sisi ili aweze kutembea maili moja akiwa amevaa viatu vyetu.
Waebrania 4:16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Kwasababu yeye alitembea maili moja akiwa amevaa viatu vyetu, sisi tunaweza kukikaribia kiti chake cha enzi, sio kiti cha hukumu bali ni cha neema, si kwa hofu bali kwa ujasiri, tupate rehema, tupate neema, tupate msaada muda ule tunapouhitaji. Haleluya!
Lakini fikiria kwanza – jaribu kuangalia ingekuaje – kama watu tunaokutana nao maishani wangeweza kutujia wewe na mimi kwa tumaini kama hilo. Ingekuaje kama wangejua kwenye kiini cha mioyo yao kwamba wakitujia, watakuwa wameingia eneo, si la kuhukumiwa, bali lenye huruma, neema na msaada!?
Kujikumbusha: uwe eneo la neema ili wengine waweze kukaribia wakiwa na ujasiri.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.