... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Huu Ndio Uweza Wako

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 3:12,13 Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi.

Listen to the radio broadcast of

Huu Ndio Uweza Wako


Download audio file

Nilishangaa mno hivi karibuni, Ong aliniambia hivi, “Nimechoshwa kusikia namna watu wanavyosema ‘kiwango cha hisia kimekuwa dhaifu.” Aa jamaniiii! Hapana, hisia za mtu zikitumika kwa akili huwa ni uweza mkubwa!”  Sijui kama umenielewa!

Angalia, sote tunatofautiana.  Kwa mimi, hata kama kiwango changu cha akili kiko sawa, daima nilikuwa ninafikiri kwamba kiwango changu cha hisia hakiko vizuri. 

Kumbe, nimejihukumu vikali kuliko watu wanavyoniona.  Lakini sisi sote tuna mapungufu kwenye tabia zetu, kila mmoja wetu ni rahisi sana kujaribu kutoa sababu za mapungufu yetu huku tukitania na kuleta udhuru. 

Ninataka kuwa muwazi kabisa,  Daima nilidharau kiwango cha hisia zangu ili niwe na udhuru hapo nilipojaribu kwa moyo wangu wote kuishi kama Neno la Mungu linavyoniongoza.  Wewe vipi?  Tafakari yafuatayo: 

Wakolosai 3:12,13  Basi, kwa kuwa mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao, jivikeni moyo wa rehema, utu wema, unyenyekevu, upole, uvumilivu, mkichukuliana, na kusameheana, mtu akiwa na sababu ya kumlaumu mwenzake; kama Bwana alivyowasamehe ninyi, vivyo na ninyi. 

Muda umewadia wa kuacha kutoa udhuru kwa ajili ya mapungufu yetu – kwa kuwa tu wateule wa Mungu, tukipendwa naye, watu wake watakatifu.  Ukisoma mistari hiyo ya Maandiko, unaona inalenga nini?  inalenga kuwa na akili katika hisia zako.  Kuwa na moyo wa rehema.  Kuwa mtu mwema, mnyenyekevu, mpole, mvumilivu.  Si mtu mwenye hasira, bali aliye tayari kusamehe. 

Sasa mtu anawezaje kukua ki-hekima katika hisia zake?  Anzia hapo hapo katika Neno la Mungu.  Halafu, acha kutoa udhuru, 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.