Fursa ya Kufanya Kazi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mhubiri 5:12 Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au kwamba amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.
Kama ungekuwa na hiari ya kuchagua kati ya kufanya kazi ngumu kwa fani ambayo unayoijua vizuri, au kuishi maisha ya anasa na starehe tu, ukifanya chochote kile unachokitaka, ungechagua maisha gani?
Kwa kawaida, wengi wangechagua maisha ya starehe, hebu fikiria, hungekuwa na haja ya kuwajibika tena. Hungekuwa na haja ya kutumika masaa marefu, hakuna tena kazi ngumu, ni kutumia muda wako wote kama unavyotaka wewe.
Naenda kasi kuelekea miaka sitini na tano sasa, muda ambao wengi wanaopenda kustaafu. Lakini nikitazama kukaa tu bila kazi, hainipendezi.
Watu wengi wanafikiri kwamba kazi ni basi tu, mchoko usioepukika ili mradi mtu na familia yake wapate riziki. Lakini kadiri ninavyozeheka, ndivyo ninavyoona kwamba kufanya kazi, kwa kweli ni fursa kubwa. Na mtazamo huo unaenda sambamba na Biblia.
Mhubiri 5:12 Usingizi wake kibarua ni mtamu, kwamba amekula kidogo, au kwamba amekula kingi; lakini kushiba kwake tajiri hakumwachi kulala usingizi.
Ni dhahiri kwamba kuna siku mwili wa mtu utachoka, na itambidi apunguze kasi ya kazi na kubadilisha mfumo wake. Lakini tuwe wawazi. Biblia haielezi hata kidogo habari ya kustaafu. Na hata kama watu wanaishi miaka mingi zaidi siku hizi, hakuna kustaafu uanafunzi wa Yesu Kristo.
Kama unaweza kutoka kwenye ajira ili ufanye kazi ya Ufalme wa Mungu muda wako wote, ni jambo jema kabisa. Lakini Mungu harefushi maisha yetu hapa duniani ili tuelekee kaburini kwa starehe tu. Anaendelea kutupa uhai ili tuweze kuendelea kuwaambia watu habari za Yesu.
Usingizi wake kibarua ni mtamu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.