... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Hata Wewe Pia Umechanganikiwa?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 1:36,37 Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Hata Wewe Pia Umechanganikiwa?


Download audio file

Najua kwamba kuna watu wengine wanafikiri kwamba mimi nimechanganikiwa.  Labda wako sahihi.  Kwa sababu ninayo dhana isiyoeleweka kwamba Mungu anaweza kufanya lolote lile, hata jambo ambalo haliwezikani kabisa; 

Wakati Mungu alipokuwa anamwambia Mariamu kwamba yeye, kama bikiria, atamzaa Yesu aliye Masihi, Mwokozi wa ulimwengu … malaika Gabrieli aliongeza neno hili pia: 

Luka 1:36,37  Tena, tazama, jamaa yako Elisabeti naye amechukua mimba ya mtoto mwanamume katika uzee wake; na mwezi huu ni wa sita kwake yeye aliyeitwa tasa; kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu. 

Matukio mawili yasiyowezekana kutokea wakati mmoja: bikira pamoja na mwanamke mzee aliyepitwa na wakati wa kuzaa, sasa wote wawili wataenda kuzaa watoto.  Yanawezekanaje?  Kuna jibu la moja kwa moja … hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.  

Sawa, tunaweza kuamini hayo yalitokea zamani, miaka elfu mbili iliyopita katika nchi ya mbali sana.  Unajua, ni rahisi kuamini yasiyowezekana yaliyoandikwa ndani ya Biblia. 

Nina kumbuka miaka mingi iliyopita, wakati niliingia katika ofisi ndogo ya huduma yetu jijini Sydney na kuiambia timu yetu ndogo ya kimataifa kwamba tutapeleka mafundisho ya Biblia kwenye bara la Afrika.  Kwetu ilikuwa haiwezikani kama vile kujaribu kuruka na kufika sayari ya Mars.  Kama nilivyosema, kuna baadhi ya watu ninaowajua wanafikiri kwamba nimechanganikiwa. 

Lakini leo hii, tunashirikisha watu ma-miliyoni kote Afrika, upendo wa Kristo kupitia vyombo vya habari na njia za mawasiliano.  A.W. Tozer alieleza hivi:  Mungu anawatafuta wale ambao anaweza kufanya kazi na kutenda yasiyowezekana – ni jambo la huzuni kwamba sisi tunapanga vitu ambavyo tunavyoweza kutimiza peke yetu. 

Hakuna lisilowezekana kwa Mungu!  Hata moja. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.