Hisia ya Kuwa na Hatia
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 3:23,24 Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.
Kuna mambo mengi yaliyo dhahiri katika maumbile ya kila mmoja wetu kwa sababu yameumbika ndani yetu kwa kuwa tumeyarithi kutokana na vizazi vilivyotangulia. Lakini kuna kitu kingine tulichokirithi kisicho dhahiri: ni hisia isiyoondoka kwamba tuna hatia.
Labda unaweza kusema, Mimi sijajisikia kuwa na hatia kubwa. Labda ndivyo ilivyo, lakini kwa kuwa siku hizi fikra zetu zimekuwa tofauti na jinsi zilizokuwa zamani katika ulimwengu huu wa sasa wenye ubinafsi, ningeshangaa kusikia kwamba hujawa na hisia mara kwa mara, kwamba hufai kutokana na mzizi wa hatia uliomo ndani yako.
Kuna sababu mtu hawezi kukosa kusikia hatia. Ni kwa sababu doa la dhambi iliyo uasi dhidi ya Mungu, tumeirithi kutoka kwa vizazi vya kale. Ukweli ni huu, kwamba …
Warumi 3:23 Kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
Mtu hawezi kukwepa ukweli huo. Ndiyo maana hisia ya hatia na kutokufaa haiwezi kutuondoka kamwe. Watu wote wamepungukiwa na utukufu wa Mungu kwa sababu ya dhambi, lakini …
Warumi 3:24 Wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu.
Wakati mtu anaamua kumwamini Yesu, karama bure ya neema ya Mungu ilionunuliwa kwa damu ya msalaba wake inamwosha mtu na kuondoa hatia kabisa kwa kuwa gharama aliyolipa Yesu kwa ajili yake inampa msimamo mzuri mbele za Mungu. Ni karama bure! Je! Tunawezaje kujua hayo? Ni kwa sababu …
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.