... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Imani kwa Ajili ya Siku Zijazo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 11:13-16 Hawa wote wakafa katika imani, wakiwa hawajazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi. Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe. Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea.

Listen to the radio broadcast of

Imani kwa Ajili ya Siku Zijazo


Download audio file

Je!, umewahi kuhisi kwamba ahadi za Mungu zimekukwepa?  Kwa kweli unatamani kusimama imara kwenye ahadi zake, lakini kwa njia moja au nyingine, hazionekani kwako.  Kama ni hivyo, basi, nikwambie kwamba hauko peke yako.

Kuna sababu inayoplekea kuwa hivyo. Unaona, wewe na mimi, katika madhaifu yetu ya kibinadamu, tunataka kuamini kwenye kiini cha mioyo yetu kwamba ahadi zake Mungu, lazima zitulenge sisi tu.  Kwamba lazima zikubaliane na ratiba ya maisha yetu.  Lakini kama mtu angetulia kwanza na kutafakari kidogo, angegundua kwamba Mungu huyu ambaye kwake miaka elfu ni kama siku moja, hatendi kazi hivyo. 

Lakini hatutaki kututulia wala hatutafakari.  Hili ndilo kosa tunalolifanya.  Kwa hiyo turekebishe mtazamo wetu.  Ebu tuangalie “ahadi za Mungu” tukiwa na mtazamo wake yeye. 

Waebrania 11:13-16  Hawa wote wakafa katika imani, wakiwa hawajazipokea zile ahadi, bali wakaziona tokea mbali na kuzishangilia na kukiri kwamba walikuwa wageni, na wasafiri juu ya nchi.  Maana hao wasemao maneno kama hayo waonyesha wazi kwamba wanatafuta nchi yao wenyewe.  Na kama wangaliikumbuka nchi ile waliyotoka, wangalipata nafasi ya kurejea. 

Ahadi za Mungu ni kubwa mno na bora kuliko yale yote ambayo tungetazamia kutokana na mtazamo wetu finyu.  Huu ndio ufunguo wa kuelewa ahadi zake.  Huu ndio ufunguo wa kuishi katika ahadi zake.  Uwe na mawazo mapana kabisa! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy