Je! Nina Haki Zote? La!
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Korintho 8:9-13 Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu. Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na ujuzi, umeketi chakulani ndani ya hekalu la sanamu, je! Dhamiri yake mtu huyo, kwa kuwa yu dhaifu, haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu? Na yule aliye dhaifu aangamizwa kwa ujuzi wako, naye ni ndugu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo. Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.
Siku hizi kuwa na dhana ya kusema “Nina haki zote!” imeenea katika tamaduni zetu, wengine wanasoma Biblia wakiwa na mtazamo huo. “Siwezi kuzuiliwa, nina haki zote!” Sasa mausia ya Mungu wanayachukulia tofauti kabisa.
Nafikiri jamii hazijawahi kuwa na migogoro mikubwa kama ilivyo leo, na hata ndani ya kanisa kuna vikundi na migogoro. Lakini hata zamani kwenye karne ya kwanza baada ya Kristo mabishano yalikuwepo na migawanyiko pia. Mtume Paulo aliandika hivi:
1 Korintho 8:9-13 Lakini angalieni huu uwezo wenu usije ukawakwaza wale walio dhaifu. Kwa maana, mtu akikuona wewe uliye na ujuzi, umeketi chakulani ndani ya hekalu la sanamu, je! Dhamiri yake mtu huyo, kwa kuwa yu dhaifu, haitathibitika hata yeye naye ale vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu? Na yule aliye dhaifu aangamizwa kwa ujuzi wako, naye ni ndugu ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake. Hivyo, mkiwatenda dhambi ndugu zenu na kuitia jeraha dhamiri iliyo dhaifu, mnamtenda dhambi Kristo. Kwa hiyo, chakula kikimkwaza ndugu yangu, hakika sitakula nyama hata milele, nisije nikamkwaza ndugu yangu.
Kadiri mtu anavyosoma Biblia ndivyo anavyozidi kufikia maamuzi ya kusema kwamba, haki tunayoweza kubaki nayo ni kukubali kuachana na mtazamo wa kudai haki zetu na kuwatanguliza wengine kwa ajili ya Kristo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.