Jinsi ya Kutokufeli
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yohana 5:19 Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
Je! Umewahi kuanza kupiga hatua ya kumtendea Mungu kazi fulani kwa imani, ukijaa ujasiri na bidii lakini kumbe, badala ya kufaulu unaanguka vibaya?! Hata mimi imenitokea. Hapo ndipo tunajiuliza kwa nini Mungu hakutuonekania. Bwana, ulikuwa wapi? Nilikutegemea sana lakini umenifelisha!
Mawazo kama hayo ni kawaida kwa watu waliothubutu kumtendea Mungu kazi kubwa lakini wakafeli. Lakini Yesu kamwe hakufeli kwa lo lote. Hata kama alionekana kuwa mwenye kufeli kuliko wote akitundikwa pale msalabani – kumbe! Ilikuwa ushindi mkubwa kuliko wote katika historia ya binadamu.
Ni kweli, kuna wakati mipango yake Mungu hua inahusisha mambo ambayo kwa mtazamo wa kibinadamu yanaonekana kuwa kushindwa, lakini kwa mtazamo wa huko juu mbinguni bado ni sehemu ya mpango wake. Pia kuna mara tumeanza kufanya kitu kwa imani, hata imani kubwa sana bila kumshirikisha Mungu ili tujue kama yale tunayothubutu kufanya kama kweli ni sehemu ya mpango wake yeye.
Sasa hapo inabidi tuulize siri yake Yesu kufaulu asilimia mia (100%):
Yohana 5:19 Mwana hawezi kutenda neno mwenyewe ila lile ambalo amwona Baba analitenda; kwa maana yote ayatendayo yeye, ndiyo ayatendayo Mwana vile vile.
Kamwe Yesu hakushindwa kumponya mtu aliyekusudia kuponya. Hakuzama wakati alitembea juu ya maji. Wakati aliagiza kwa ujasiri maji yabadilike kuwa divai, ilitokea hivyo hivyo. Kwa sababu gani?
Ni kwa sababu daima alitenda lile ambalo aliliona Baba akilitenda tu. Alikaa katika mapenzi ya Baba yake. Kwa hiyo, ukitaka kupiga hatua katika imani, hakikisha kwanza kwa kumshirikisha Mungu. Omba, tafuta mapenzi yake ili hatimaye ufanye yale tayari Baba anayatenda!
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.