Jua Ukweli Uko Wapi, Lakini …
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 4:7,8 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
Kumbe, ukweli unaweza kuleta hatari kama ukitumiwa vibaya, kama vile kisu kikali kinavyoweza kuua endapo kikitumiwa kwa hasira. Ndivyo ilivyo Injili ya Yesu. Saa wali ni hili, unaitumiaje!?
Profesa maarufu wa saikolojia kutoka Canada aitwaye Jordan Peterson, yeye ni mtu anayepinga fikra za watu. Haijalishi unamchukuliaje, yeye bado anasema kwamba itikadi huwa inawekwa badala ya elimu ya kweli, kwa hiyo ni hatari sana pale watu wenye itikadi wanapoingia madarakani, kwasababu mtazamo wa kufikiri kwamba “mimi nimeshajua kila kitu” hauwezi kukabiliana na changamoto za maisha haya.
Sasa kuna hatari kwa yule anayemwamini Yesu, anayejua ukweli wa Injili ya Kristo, anaweza kubadilisha amali ya upendo iliyo katika imani ndani ya Yesu kuwa itikadi. Hatari ni kwamba sisi tunakuwa wenye itikadi, tukiwapiga watu kwa kutumia kweli.
Sisi sote, tumeshuhudia namna itikadi inafukuza watu wengi wasije kwa Yesu. Maisha ni mchanganyiko wa changamoto nyingi sana, watu wakitawaliwa na dawa za kulevya, wengine kutengwa na jamii, mazingira magumu yasiyoelezeka. Kwahiyo, nadhani muda umewadia … nisemeje … ni muda mwafaka wakusikiliza Neno linalotoka kwa Mfadhili wetu Mkuu:
1 Yohana 4:7,8 Wapenzi, na mpendane; kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu, na kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
mimi binafsi nilijikuta katika hali ngumu mno, si Wakristo walionichapa kwa kutumia ukweli ambao kwahuo walinivuta kwa Yesu, la! Bali kilichonivuta ni upendo wa Wakristo.
Yeye asiyependa, hakumjua Mungu, kwa maana Mungu ni upendo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.