... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Juu umbali Gani? Mbali urefu gani Gani?

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Zaburi 103:11,12 Maana mbingu ziivyoinuka juu ya nchi, kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao. Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi.

Listen to the radio broadcast of

Juu umbali Gani? Mbali urefu gani Gani?


Download audio file

Maisha huwa yanatabia ya kuchokonoa imani ya mtu.  Yaani, visiki na vikwazo, majaribu na mivutano, yaani tuseme, matope ya maisha – hayoyote yanaweza kuondoa macho yetu tusimtazame Yesu tena bali tuangalie matatizo yaliyoko mbele yetu tu.

Bila shaka umeshapitia hayo, sindiyo?  Ni kweli, unafahamu kwamba Mungu alikupenda kiasi cha kumtuma Yesu kufa kwa ajili yako.  Lakini maisha ni magumu.  Kuna wakati tunapambana kabisa, kuna siku tunachoshwa na kazi za kila siku, kuna wakati tunapata vishwawishi vya kutupotosha.  Hayo yote yanatukusanyikia kuondoa macho yetu kwenye upendo wa ajabu wa Mungu. 

Muda umewadia wakutulia kwanza, turejee tena, tumpe nafasi Mungu Roho Mtakatifu aweze kuvuta macho yetu tumtazame yeye. 

Zaburi 103:11,12  Maana mbingu ziivyoinuka juu ya nchi, kadiri ile ile rehema zake ni kuu kwa wamchao.  Kama mashariki ilivyo mbali na magharibi, ndivyo alivyoweka dhambi zetu mbali nasi. 

Fadhili za Mungu kwako ni kubwa mno! Ni kama mwinuko wa mbingu juu yetu.  Kama ungeruka angani na roketi huwezi kufikia mbingu.  Ndivyo fadhili za Mungu zilivyo juu sana.  Ndivyo uaminifu wa fadhili zake zilivyo kwako. 

Sasa ameweka dhambi zako na udhalimu wako mbaya, mbali na wewe kiasi gani?  Hata ukianza kusafiri kuelekea mashariki na mimi kuelekea magharibi, hatuwezi kukutana nazo.  Hata kama maisha yakusumbuaje, usipoteze maono ya upendo wa milele Mungu aliynayo kwa ajili yako. Kamwe usisahau gharama inayotisha aliyolipa ili aondoe kabisa dhambi zako. 

Unapendwa na upendo wa milele.  Umesamehewa kabisa kabisa … kupitia Yesu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy