Kanuni ya Msingi Katika Mawasiliano
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Peter 3:14,15 ... Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwengu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.
Jana tuliongelea swala la ukosefu wa adabu siku hizi katika majadiliano ya jamii na nafasi nzuri tulizo nazo, wewe na mimi kwa kurejesha ustaarabu kwa kutumia maneno ya kujenga, yenye neema pamoja na kujaribu kuwaelewa watu wengine.
Lakini katika mazingira ya watu wanaojaribu kunyamazisha Wakristo na kutenga Mungu wetu wa Biblia na maagizo yake yote kwasababu yanawasumbua, ni rahisi mfuasi wa Kristo kujaribu kuafikiana nao na kulegeza masharti ya ukweli.
Kuendana na mkondo wa wakati au kugushi mambo magumu ili kujaribu kuvuta watu waokoke, ni kazi bure. Kuna madhehebu mengi walijaribu kufanya hivyo kwasababu ya hofu ya mashambulizi makali kutoka kwa watu wanaopinga Injili ya Kristo, baadhi wanajaribu kunyonga maneno na kugushi ukweli.
Lakini Mtume Petro aliwaandikia Wakristo waliokuwa wanaudhiwa karne ile ya kwanza, akisema hivi:
1 Peter 3:14,15 … Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwengu. Mwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa hofu.
Hapo ndipo tunapopata kanuni za msingi kuhusu mawasiliano.
Usiogope wanaokupinga, Usifadhaike, mheshimu Yesu kama Bwana, mpe nafasi ya kwanza, hapo ndipo utakaposimama imara kwenye kweli, uweze kuambia watu kwanini unatumaini kubwa kwake … lakini waambie kwa upole na heshima.
Hakuna sababu ya kuogopa. Hakuna sababu ya kughushi Injili. Hakuna sababu ya kupaza sauti na kuwapigia watu kelele.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.