Kimbia kwa Nguvu Zako Zote
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 3:13,14 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Mtu yeyote aliyedhamiria kumfuata Yesu anajua kwamba kuna siku imani inakuwa juu sana. Lakini siku zingine, imani inayumbishwa kabisa. Yaani, nikizingatia makosa yangu yale yote … nitaufikilila mwisho wa safari kweli kweli?
Acha nikwambie wazi, hauko peke yako. Yaani hali hiyo ya mashaka imeshanitokea mimi na bila shaka itanitokea tena. Pia, bila shaka imempata kila mwanamume na kila mwanamke na kila mtoto aliyewahi kukusudia moyoni huku akimwamini Yesu na kumfanya awe Bwana wa maisha yake. Hata Mtume Paulo aliyeandika nusu ya vitabu vya Agano Jipya alielewa hali hiyo.
Kwahiyo, kama unayumbishwa kwa kutazama yaliyopitika kwenye maisha yako – hata kama ulikuwa na mapungufu gani na makosa mengi – kama hayo yote yanakulemea, basi hapa kuna Neno la Mungu linaloweza kukutia moyo leo:
Wafilipi 3:13,14 Ndugu, sijidhanii nafsi yangu kwamba nimekwisha kushika; ila natenda neno moja tu; nikiyasahau yaliyo nyuma, nikiyachuchumilia yaliyo mbele; nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.
Unaona? Paulo alifahamu kwamba alikuwa hajakamilika. Sasa alifanyaje? Alisahau yaliyo nyuma na aka chuchumilia yaliyo mbele. Aliamua kupiga mbio kama mwanariadha; kutumia nguvu zake zote kumaliza mwendo na kushindia tuzo.
Rafiki yangu, yaliyo nyuma yamepita, Huwezi kuyabadilisha tena. Kaza macho kwenye mwisho wa mashindano.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.