Kisasi Kizuri
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Warumi 12:17-19 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
Mtu akikudhulumu au akimdhulumu rafiki yako, halafu hasira yako ikipanda mpaka kugadhibika, je! Ni kitu gani unachotaka kufanya kuliko vyote? Kujilipiza kisasi. Ingekuwa tamu kwako kabisa.
Labda inaeleweka vibaya lakini kuna sababu mtu anataka kujilipiza kisasi. Ni kwa sababu ameumbwa kwa sura yake Mungu, kwa hiyo hisia yake ya kutafuta haki inasimama kinyume ya uonevu unaomkabili.
Haki inadai kwamba uonevu wote ukomeshwe, mambo yatengenezwe. Haki inadai kwamba aliyedhulumu aadhibiwe tena alipe fidia. Na hii ndiyo maana Yesu alikufa pale msalabani kwa ajili yako na kwa ajili yangu; ili akomeshe makosa yetu; abebe adhabu tunostahili sisi.
Kwa hiyo, Mungu, badala ya kujilipiza kisasi yeye mwenyewe kwa kuwa tumemwasi, yeye alilipa deni la dhambi zetu kupitia kifo cha Yesu pale msalabani na kumaliza madai ya haki. Ukitafakari kidogo, utaona kwamba ni mwitikio wa ajabu mno dhidi ya makosa tuliyomtendea. Mwitikio huo umetokana na pendo lake kwetu.
Yamkini, ni bora tumwachie yeye swala zima la kisasi:
Warumi 12:17-19 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
Ina maana, kujilipiza kisasi kuzuri ni kuachia tu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.