Kitendawili cha Uhuru
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wagalatia 5:13 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.
Sisi sote tunayo shauku ya kuwa huru, huru kutoka kwenye kanuni, mizigo , majukumu yanayotuelemea, huru kutoka kwenye mahusiano yanayosumbua. Ni mambo mengi tu ambayo tungependa kuwa huru nayo.
Kwa mtu ambaye daima amekuwa na mapungufu ya kiuchumi, jamani na matizo mbalimbali ya kwenye ndoa angejisikia amani kama atakuwa huru, angejisikia huru kabisa kama angeweza kuachana na mwenzie na kuendelea na maisha akiwa na wepesi.
Kwa kweli, Mungu ametuchagua tuwe huru ila, aina ya uhuru aliyotuandalia pengine si uhuru ule tuliokuwa tunautazamia.
Wagalatia 5:13 Maana ninyi, ndugu, mliitwa mpate uhuru; lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.
Uhuru ambao Mungu anauzung’mza hapo ni uhuru kutoka kwenye tamaa mbaya ,dhambi na kutoka kwenye matokeo ya udhalimu wetu wote. Pia, tukisema ukweli, yale yote mengine ambayo nimeyataja hapo juu , yangeweza kutupelekea kutenda yasiyofaa , kutumia uongo, kuachana na mwenzi na kufanya mengi yasiyo na haki.
Wakati mtu anamwamini Yesu, anawekwa huru na mzigo wa dhambi zake wenyewe. Huu ndio uhuru wa kweli. Ni uhuru unaomweka mtu huru licha ya matatizo yote yanayomsonga. Kwa hiyo …
Maana ninyi ndugu mliitwa mpate uhuru,lakini uhuru wenu usiwe sababu ya kuufuata mwili, bali tumikianeni kwa upendo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.