Kuamini Bila Kusitasita
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wakorintho 13:7 Upendo huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
Je! Umewahi kuchoshwa na mtu fulani, au mtu ambaye mmekuwa marafiki kwa muda Haujambo? Mimi ni Berni Dymet na ninakukaribisha kwenye kipindi hiki cha NENO SAFI NA LENYE AFYA.
Nadhani sisi sote tunamarafiki kama hawa. Basi! Sitamwalika tena kwetu! Au mwanamke yule uliyekuwa rafiki yako miaka mingi, lakini anazidi kukusumbuana. Imefika mahala, unamtenga ukisema, “Kweli hanifai tena!”
Sasa, tunawezaje kufikia maamuzi kama hayo? Inawezekanaje kumtupa kama takataka, mahusiano ambayo yalikuwa muhimu kwetu?
Labda maneno yangu yamekuumiza leo au nimetonesha jeraha. Lakini, inawezekana jeraha litakuwa kimepata tiba leo hii. Labda Andiko hili linaweza kuwa Neno la kukufaa leo.
1 Wakorintho 13:7 Upendo huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
Hata Mimi na wewe, tuliwahi kusumbua watu wengine wanaotuzunguka? pia tuliwahi kuchukiza wenzetu wakati tulikuwa tunapitia vipindi vigumu, si kweli?
Lakini bado wale watu waliendelea kutujali.
Upendo huvumilia yote; huamini yote; hutumaini yote; hustahimili yote.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.