... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuachana kwa Talaka (1)

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Malaki 2:13-16 Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia. Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani? Ni kwa sababu BWANA amekuwa shaidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, angawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako. Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo. Au je! Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu? Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana. Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana.

Listen to the radio broadcast of

Kuachana kwa Talaka (1)


Download audio file

Uasherati na kupeana talaka siku hizi ni kama kawaida, watu wanafikiri kwamba haina shida, kwamba ni hiari ya mtu badala ya kuviona kuwa usaliti na kutenda mambo ya hiana. Lakini havikukusudiwa hata siku moja!

Ninaongea kama mtu ambaye mke wake wa kwanza alimwacha kwa ajili ya mwanaume mwingine, mtu ambaye nilifikiri kwamba mke ni rafiki yangu wa karibu sana.  Yaani, kuachana.  Huwa inatokea. Watu wanatengana polepole hatimaye wanaachana na kutafuta mwingine. Lakini sikitiko la kutokuwa waaminifu katika ndoa ni kubwa mno na linaleta maumivu makali ndani ya mtu kwa namna isiyoelezeka.  Kwahiyo, kama umewahi kufikiri kuzini na kuacha kumpenda mwenzi wako ili ukumbatiwe na mikono ya mwingine asiye wako, Sikiliza yafuatayo: 

Malaki 2:13-16  Tena mnatenda haya nayo; mnaifunikiza madhabahu ya BWANA kwa machozi, kwa kulia na kwa kuugua, hata asiiangalie tena hiyo dhabihu, wala kuitakabali mikononi mwenu na kuiridhia.  Lakini ninyi mwasema, Ni kwa sababu gani?  Ni kwa sababu BWANA amekuwa shahidi kati ya wewe na mke wa ujana wako, uliyemtenda mambo ya hiana, ingawa yeye ni mwenzako, na mke wa agano lako.  Hakuna mtu mmoja aliyetenda hivi, ambaye alikuwa na ufahamu kidogo.  Au je!  Kuna mtu mmoja atafutaye mzao mwenye kumcha Mungu?  Kwa hiyo jihadharini roho zenu; mtu awaye yote asimtende mke wa ujana wake mambo ya hiana.  Maana mimi nakuchukia kuachana, asema BWANA Mungu wa Israeli; naye aifunikizaye nguo yake kwa udhalimu namchukia, asema BWANA wa majeshi; basi jihadharini roho zenu, msije mkatenda kwa hiana. 

…. hata wewe mama, usimtendea kwa hiana mume wako.  Nyote msithubutu! 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.