... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kutengana Bila Mwelekeo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wimbo Ulio Bora 2:15 Tukamatie mbweha, wale mbweha wadogo, waiharibuo mizabibu, maana mizabibu yetu yachanua.

Listen to the radio broadcast of

Kutengana Bila Mwelekeo


Download audio file

Familia zetu ni muhimu sana kwenye maisha. Lakini familia nyingi zina matatizo kweli. Familia nyingi wanazo “ishu” nyingi tuseme. Pia, na ni huzuni kabisa kulisema, familia nyingi zimeshasambaratika.

Lakini kwa familia zile ambazo bado wanapambana na changamoto, Itakuwaje?  itakuaje pia kwa familia ambazo tayari wameshatangua ndoa?  Au pale mmoja amezini?  Au…Sijui kama unanielewa?  Sasa kwa watu kama hawa, itakuaji?  Kwahiyo, leo na wiki mbili zinazofuata kwenye kipindi chetu cha Neno Safi na Lenye Afya, tutasimulia hayo hayo.  Familia ambazo bado wanapambana.  Familia zilizosambaratika. Watu ambao hawajaoa au kuolewa.  Mambo mengi tu ambayo mara nyingi huwezi kuyasikia yakizungumzwa, hususani katika jamii za Wakristo. 

Tuanze na hali halisi ya jambo hili: 

Wimbo Ulio Bora 2:15  Tukamatie mbweha, wale mbweha wadogo, waiharibuo mizabibu, maana mizabibu yetu yachanua. 

Kuna ndoa nyingi sana zinaanza kusambaratika kwasababu ya mambo madogo-madogo,  Kumchezea mwingine asiye mke wako au mume wako.  Kuruhusu udhia na kero kukutenganisha na mpendwa wako.  Kuzembea na kuacha kutenga muda wa kutosha kwa ajili ya kuwa na mwenzi wako.  Kujali simu yako ya mkononi kuliko anayotaka kusema mpendwa wako. 

Kutokujaliana ni chanzo cha familia yako kusambaratika.  Usiruhusu hali hii kuendelea. Kwahiyo, wajibika! chukua hatua! 

Tukamatie mbweha, wale mbweha wadogo, waiharibuo mizabibu, maana mizabibu yetu yachanua.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.