Kuielewa Neema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 2:17-19 Walipomwona wakatoa habari waliyoambiwa juu ya huyo mtoto. Wote waliosikia wakastaajabu kwa hayo waliyoambiwa na wachungaji. Lakini Mariamu akayaweka maneno hayo yote, akiyafikiri moyoni mwake.
Ni usiku wa kuamkia Krismasi, Muda umewadia wa kuwa makini kukumbatia mioyoni mwetu na hata katika fikra zetu, ukweli mkubwa sana, ukweli usioelezeka wa neema ya Mungu kwa kila mmoja wetu kupitia Mwanawe Yesu Kristo.
Kuna kitu kimoja cha msingi kinaweza kuelekeza maisha yako vizuri. Ni kukumbuka ya mambo muhimu, Kwa sababu ni kama vibao vya barabarani vinavyokuongoza katika maisha yako ili vikufikishe panapotakiwa.
Ndoa zinavunjika kwasababu mume na mke wanasahau umuhimu wa mwenziwe. Hawaangalii tena kibao kile kilichohusu ndoa yao na kwa hiyo wanaanza kuachana mapema.
Hivyo hivyo, hata kama unakiri kwamba una imani ndani ya Yesu, kwamba yeye ndiye jiwe kuu la pembeni katika msingi wa maisha yako, uhai wako kwa ujumla, bado unaweza kupelekwa mbali naye katika mwenendo wako kama huna kumbukumbu za neema yake kwako, neema isiyoelezeka.
Ndio maana Krismas ni kipindi muhimu sana. Ni muda mzuri wa kusimama, kutulia, kukumbuka na kushukuru kwaajili ya neema yake. Kama vile walivyofanya wale wachungaji baada ya kumtembelea Yesu katika zizi lile akiwa horini.
Luka 2:20 Wale wachungaji wakarudi, huku wanamtukuza Mungu na kumsifu kwa mambo yote waliyosikia na kuyaona, kama walivyoambiwa.
Ebu fikiria kama ungekuwa unatembea nao wakitoka kijiji cha Bethlehemu kurudi kwenye mifugo yao, msisimko wao ulikuwaje? Mshangao mkubwa, furaha kuu. Walivyotembea kwa ufahari wa yale waliyoyashuhudia. Kamwe usisahau kumtukuza Mungu, kumshukuru kwaajili ya yote aliyokutendea ndani ya Mwanawe Yesu Kristo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.