Kuleta Faraja
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Wafalme 19:5,6 Naye Eliya akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena.
Kuna wakati unaweza kujikuta kwenye shimo ndefu lenye giza. Huwa inatokea maishani. Mashimo yale yanatofautiana kwa saizi lakini ni kama ni marefu, yenye giza.
Ni lini uliwahi kujikuta kwenye shimo kama hilo? Je! ilitokana na makosa yako mwenyewe!? Au labda ni matokeo ya mazingira yaliyokuwepo nje ya uwezo wako?
Haijalishi imesababishwa na nini, bado shimo ndevu lenye giza ni sehemu ya kutisha. Halafu watu wenye nia njema wanakuja na kukuhubiri, hata kukulaumu kana kwamba ingesaidia lolote.
Lakini Mungu anapoona kwamba mmoja wa watoto wake ameanguka shimoni, kwa kweli yeye anatumia njia tofauti kabisa.
1 Wafalme 19:5,6 Naye Eliya akajinyosha akalala chini ya mretemu; na tazama, malaika akamgusa, akamwambia, Inuka, ule. Akatazama, kumbe! Pana mkate umeokwa juu ya makaa, na gudulia la maji, kichwani pake. Akala, akanywa, akajinyosha tena.
Kama vile mtu fulani alivyosema, Eliya alipokuwa anakatishwa tamaa mno, Mungu hakutuma malaika kumhubiria, kumwambia azidi kuomba, wala hakumhukumu kwa sababu ya hali yake, bali alimtuma malaika kumfariji pale alipopumzika.
Tukijaribu kuwaelewa wanaotuzunguka, tutagundua kwamba baadhi ya wale wanaoumia au waliopata hasara wanahitaji faraja tu. Halafu siku za karibuni, malaika atakayetumwa kwao si mwingine, yamkini atakuwa wewe au mimi.
Kuna watu wanahitaji kufarijiwa, basi.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.