Kulipiza Kisasi au Kumrejesha Ndugu?
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mathayo 18:15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
Je! Ni muda gani tangu ulipofedheheshwa, au kutengwa, au kutendewa visivyo?
Haijashi ni sababu gani, hali hii hua inatokea mara kwa mara, si kweli? Labda ni kitu kidogo kama vile rafiki au jamaa kuchosha kwa kukaa sehemu moja kwa muda mrefu ni kitu kinachoumiza mno, mfano wakati mtu wa karibu anakusaliti.
lakini kwa vyovyote, kinachochea ndani yetu ni hisia kwamba hatukutendewa haki – Mimi sistahili kutendewa hivyo! Bila shaka umewahi kujisikia hivyo, Tumsikilize Yesu:
Mathayo 18:15 Na ndugu yako akikukosa, enenda ukamwonye, wewe na yeye peke yenu; akikusikia, umempata nduguyo.
Maneno hayo, lazima yazue maswali ya msingi, kwa kuwa yametamkwa na yule aliyeshuka hapa duniani ili atuokoe wewe na mimi tusitengwe na Mungu milele kwa sababu ya dhambi zetu.
Wakati mtu anatudhulumu, je! Tunatafuta kujilipiza kisasi au tunatafuta ule upatanisho? wakati mtu fulani aliyekusumbua … je! Mwitikio wako ulikuaje? Ulijaribu kujilipiza kisasi kwa sababu uliona kwamba umeonewa, au ulikuwa na shauku ya kurejesha uhusiano mzuri naye?
Ikiwa mtu amekukosea, mwambie – faraghani na kwa utaratibu na upole. Akikusikia, umempata nduguyo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.