... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kukabiliana na Lawama

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mithali 15:31,32 Sikio lisikilizalo lawama yenye uhai litakaa kati yao wenye hekima. Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu.

Listen to the radio broadcast of

Kukabiliana na Lawama


Download audio file

Unyumbukaji, yaani kuwa mwepesi kupokea maonyo na kujirekebisha, ni tabia inayotupasa kufundisha watoto wetu wakiwa bado nyumbani kwa sababu huko mbeleni, maisha yatawawia vigumu.  Lakini sisi wenyewe, je!  Tuko tayari kurekebika na kupokea maonyo?  Je!  Tunakabilianaje na ukosoaji?

Mwaka 2019, katika Gazeti ya Biashara ya Harvard, mwandishi maarufu na mwanasayansi wa kijamii, Joseph Grenny aliandika hivi:  Hata kama ukosoaji unaletwa kwa upole – na kwenye utandawazi ni mara chache sana unaoletwa hivi – unaweza kutisha hitaji ya saikolojia ya mwanadamu kuwa salama. Sasa kukabiliana na lawama kwa njia ya kuirudia hali ya uthabiti, inatakiwa mtu ajitenge na maneno yale ya ukosoaji ili akwepe hisia za kutokufaa na haja ya kujihami. 

Na hoja ni hapo hapo, sindiyo?  Hata lawama yenye uhai ya kutusaidia inatutikisa mpaka ndani ya kiini cha nafsi yetu.  Hata mkosoaji akiwa na lengo zuri, bado hisia zetu zinatuvuruga hadi tunataka kujihami.  Ndipo tunapata hasara ya kutokufaidika na mafao makubwa ambayo yangeletwa na maonyo yale mazuri. 

Mithali 15:31,32  Sikio lisikilizalo lawama yenye uhai litakaa kati yao wenye hekima.  Akataaye maonyo huidharau nafsi yake mwenyewe; bali yeye asikilizaye lawama hujipatia ufahamu. 

Yaani mwandishi huyu hakukwepa jambo, si kweli?  Ili tupate hekima, lazima tujifunze kupokea ukosoaji, na kutathmini mambo kwa ukweli na uwazi, ili tujue kama lawama zile ni za kweli.  Kama ziko sahihi, ni kuzifanyia kazi – bila kuogopa, bila kusita.  Kwa sababu tukikataa maonyo mema, sisi wenyewe tutakula hasara. 

Sikiliza ukosoaji – uupokee na kuufanyia kazi – na utazidi kupata ufahamu.  Hatimaye utahesabiwa kuwa mmoja wa watu wenye hekima. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.