... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Maisha ya Uzima Tele

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favourites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waefeso 3:16-19 Awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani. Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Maisha ya Uzima Tele

Download audio file

Kuna utofauti mkubwa kati ya maisha ya uzima tele na maisha tupu, maisha yanayobariki wengine na yasiyobariki , maisha ya kuridhisha kabisa na maisha ya mahangaiko tu.  Je!  Wewe unaishi maisha gani?

Ni swali linaloleta tafakuri kwa kweli kwa sababu mtu anaweza kuendelea na shughuli zake za kila siku , hatimaye akazeeka, asiwe tena na shughuli nyingi, pengine akiwa na upweke ,yaani maisha yanaendela tu bila mwelekeo hadi yanaisha. 

Hatimaye, mtu akikaribia mwisho wa maisha yake,  ndipo anagundua kwamba hakuishi maisha ya uzima tele kama alivyotadhania. 

Yesu aliahidi kwamba watu watakaomwamini bila shaka watateswa kama yeye alivyoteswa.  Haya  ni maneno mazito, lakini pia aliahidi kwamba tungeishi maisha ya uzima tele.  Kuna mtu mmoja aliniuliza maana ya kuishi “maisha ya uzima tele.”   Nilimjibu kwa kutumia maneno ya Mtume Paulo wakati alikuwa anaelezea rafiki zake. 

Waefeso 3:16-19  Awajalieni, kwa kadiri ya utajiri wa utukufu wake, kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani.  Kristo akae mioyoni mwenu kwa imani mkiwa na shina na msingi katika upendo; ili mpate kufahamu pamoja na watakatifu wote jinsi ulivyo upana, na urefu, na kimo, na kina; na kuujua upendo wake Kristo, upitao ufahamu kwa jinsi ulivyo mwingi, mpate kutimilika kwa utimilifu wote wa Mungu. 

Maisha ya “uzima tele” ni maisha ya kuwa na nguvu ya undani, Kristo akikaa moyoni mwa mtu, maisha yenye shina na msingi katika upendo, maisha katika upana ule wote wa wingi wa pendo lake Mungu kwetu.  Kwa hiyo niulize tena, je!  Unaishi maisha ya aina gani? 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy