Hekima ya Ki-Balozi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 4:5,6 Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Daima kumekuwa na msuguano wa mawazo kati ya watu wenye imani na wasio na imani na mimi ninadhani utaendelea tu, kati ya wanaomwamini Yesu na wasiomwamini. Sasa kuna njia mbili zisizo sahihi ambazo Wakristo wengi wanazitumia kwa kukabiliana na hali hiyo.
Njia moja ni kuondoa msuguano tu kwa kuinua mikono na kukubali kupelekwa na mkondo wa mawazo ya wasioamini. Njia ya pili ni kuwapigia kelele wanaopinga imani yetu na kurudisha moto kwa moto.
Juzi niliona picha ya watu wawili waliokuwa wanamtazama Yesu akitundikwa msalabani. Mmoja aliuza mwenzake, “Je! nini kilichosababisha watu wawe na jazba kiasi hicho?” Wa pili alimjibu, “Alisema, ‘Muhurumiane’.” Ndipo ule wa kwanza alisema, “Ni kweli, kusema hivyo lazima watu wachukie!”
Kusema tu, mpende Mungu, mpendane kwa ghafla anasulubiwa? Sasa huruma hiyo ina uhusiano gani kwa swala letu la msuguano kati yetu na wasioamini ambao tunaoupitia?
Wakolosai 4:5,6 Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.
Ebu fikiria kama nchi fulani ingetuma balozi kwa nchi nyingine na balozi yule mara moja anaanza kutupia nchi ile kejeli kwa sababu yeye hakubaliani na sera zao. Sidhani ni diplomasia na unahisi kitatokea nini?
Kwa mstari huu, Mungu anatwambia tuwe na hekima ya kibalozi, kama unamwamini Yesu, wewe ni balozi wa Kristo, kwa hiyo inabidi uenende kama balozi … lakini hata hivo inawezekana bado watu wanaweza kukusulubisha.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.