... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kumuonea Mungu Shauku

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Kutoka 33:18-20 Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako. Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu. Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi.

Listen to the radio broadcast of

Kumuonea Mungu Shauku


Download audio file

Kuna hamu kubwa moyoni mwa kila mtu kujua vitu; ni shauku ambayo wengi wanaitafuta lakini kwa kupapasa-papasa tu.  Shauku ambayo imo katika swala la Ukristo kwa ujumla.

Ni hamu niliyokuwa nayo kwa miaka mingi, lakini popote pale nilipotafuta, hata kwa kujitahidi sana, sikuridhika.  Ni shauku ambayo Musa alilokuwa nayo pia, yeye aliye maarufu sana katika Agano la Kale.  

Kutoka 33:18-20  Akasema, Nakusihi unionyeshe utukufu wako.  Akasema, Nitapitisha wema wangu wote mbele yako, nami nitalitangaza jina la BWANA mbele yako; nami nitamfadhili yeye nitakayemfadhili; nitamrehemu yeye nitakayemrehemu.  Kisha akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi. 

Musa alitaka amuone Mungu, alitaka awe na uhusiano naye na kumjua. Lakini Mungu alijua kwamba hata Musa, mtumishi wake, asingenusurika kwa kuangalia sura yake.  Kwahiyo Mungu alimwonyesha mengine yasiyotisha – alimuonyesha upendo wake, rehema zake, wema wake mkamilifu vitu visivyotisha kabisa. 

Pia Mungu alitumia jina lake binafsi – YAHWEH – jina ambalo Waisraeli waliliogopa kulitumia kwa sababu lilikuwa takatifu sana, hawakutaka hata kulitamka. 

Hali iliendelea kuwa hivi hadi Krismasi ile ya kwanza. Hadi wakati  uleambao Mungu alifanyika kuwa mtu ili aweze kutembea katikati yetu. Kama vile Yesu alivyojitambulisha, “Aliyeniona mimi, tayari ameshamwona Baba aliyenituma.” 

Kwahiyo, kama una shauku kubwa moyoni mwako, basi jua hili.  Jibu ni Mungu mwenyewe.  Halafu sasa … unaweza hata kuona uso wake. Yesu. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo. 


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy