... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuna Mashindano ya Kupiga Mbio

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 3:14 Nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu.

Listen to the radio broadcast of

Kuna Mashindano ya Kupiga Mbio


Download audio file

 hivi, wakati ukijiandaa kuingia mwaka mpya, je!  Utaniruhusu nikikuuliza swali?  Je!  Mede ya thawabu yako iko wapi?  Je!  Mashindano yako yataisha lini?

Labda utanishangaa kuongea habari ya kumaliza mashindano wakati tunataka kuanza mwaka mpya.  Lakini hatuwezi kukwepa swali hilo kwa sababu kila mtu ana siku atakayomaliza mashindano yake na wengi wetu hatujui tutamaliza lini wala wapi mwisho utatokea. 

Kwa hiyo tunaendelea kana kwamba hakuna mwisho wa mashindano ya kupiga mbio hapa duniani.  Lakini kuna mwisho kabisa, kwa kuwa mwili utachoka na kusalimu roho, au Yesu atarudi … kwa vyo vyote mwisho unakuja. 

Sasa, utafanya nini tangu hapo ulipo sasa na hatima ya safari yako?  Utakimbiaje mashindano yako?  Je!  Utanaswa na shughuli na mahangaiko ya maisha haya au utalenga tuzo lililowekwa mbele yako?  Kwa kuwa mwisho wa kupiga mbio unaweza kutufikia muda wo wote, tuangalie sasa mwaka huu mmoja unaotaka kuanza.  Utafanyaje mwaka mpya?  Je!  Utakaza mwendo?  Utakimbiaje?  Mtume Paulo aliandika hivi …

Wafilipi 3:14  Nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. 

Mungu ameandaa maisha ya ajabu kwa ajili yako kuanzia sasa hadi kuingia umilele.  Kaza macho huko mbeleni, piga mbio kuelekea mwisho wa mashindano, jitolee, hudumia wengine, mheshimu na kumtukuza Mungu wako.  Kwa sababu tuzo – uzima wa milele ndani ya Kristo Yesu – ni thawabu inayoridhisha.

Kaza mwendo.  Piga mbio.   

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.