... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mawazo ya Mtu Mzima

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wafilipi 3:15,16 Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo. Lakini, hapo tulipofika na tuenende katika lilo hilo.

Listen to the radio broadcast of

Mawazo ya Mtu Mzima


Download audio file

Kadiri mtu anavyojitahidi kutenda jambo la maana katika maisha haya, ndipo ataanza kutaka kupunguza kasi, kupumzika kidogo na kuruhusu mawazo yake kuzurura pengine … hatimaye kuliacha kabisa.  Sijui kama umeshaona hilo?

Jana tulisimulia habari ya mfumo mwenye nguvu aliutumia Mtume Paulo kwa jinsi alitaka kuishi muda ambao angeendelea kuwapo hapa duniani …

Wafilipi 3:14  Nakaza mwendo, niifikilie mede ya thawabu ya mwito mkuu wa Mungu katika Kristo Yesu. 

Lakini unajua kwamba kuendelea kupiga mbio kwa kukimbia ni kazi kweli, hususani huku umejitwika msalaba wako ili umfuate Yesu.  Kwa hiyo, kama umepata jaribu la kulegeza na kupunguza kasi, basi sikiliza alivyozidi kuandika Paulo: 

Wafilipi 3:15,16  Basi sisi tulio wakamilifu na tuwaze hayo; na hata mkiwaza mengine katika jambo lo lote, Mungu atawafunulia hilo nalo.  Lakini, hapo tulipofika na tuenende katika lilo hilo. 

Ni wepi wanaopaswa kuwaza hayo?  Ni wepi wangekaza mwendo?  Sisi sote ambao tumekomaa kiroho!  Yamkini leo Mungu anajaribu kukuonyesha jambo fulani muda huu huu.  Pengine ni wito wa kukuamsha na kukutia moyo kupitia nguvu za Roho muda huu unaojiandaa kuanza mwaka mpya. 

Kwa sababu kama hupigi hatua mbeleni na kukimbia kwa nguvu zote ushikilie tuzo lililowekwa tayari kwa ajili yako ndani ya Kristo, basi utakuwa unarudi nyuma katika maeneo yale ambapo Shetani, akivizia kukuiba, atakushambulia mara tena na tena.  Kwa hiyo … Hapo ulipofika na uenende katika lilo hilo.  Piga mbio kabisa hadi umalize mwendo.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.