Kurejea Habari za Ayubu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Ayubu 23:10-12 Lakini yeye aijua njia niendeayo; akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu.
Ni rahisi kuwa na matumaini ya siku zijazo pale mambo yote yanapokuwa shwari. Lakini pale mamno yanapokwenda tofauti mtu anaweza kukatishwa tamaa na kufa moyo. Na hali hiyo ni hatari.
Juzi tuliongea habari za mtu ndani ya Agano la Kale aitwaye Ayubu. Yeye alipitia matatizo mengi na makubwa lakini hakumlaumu Mungu. Ilibidi akaze moyo lakini bila shaka, kuna siku alilia machozi mengi.
Hata hivyo alisema: BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA na libarikiwe. Aliweza kustahimili hali ya kupotelewa na mali zake, kushushwa hadhi katika jamii, kufiwa na watoto wake wote kumi, yaani kila kitu … ni kwa sababu … acha aseme yeye mwenyewe:
Ayubu 23:10-12 Lakini yeye aijua njia niendeayo; akisha kunijaribu, nitatoka kama dhahabu. Mguu wangu umeshikamana sana na hatua zake; njia yake nimeishika, wala sikukengeuka. Sikurudi nyuma kuiacha amri ya midomo yake; nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu.
Aliwezaje Ayubu kustahimili mateso yake? ni kwa kutunza amri za Mungu, kuthamini Neno la Mungu kuliko mazingira yake, kuliko maumivu yake, kuliko ukosoaji wa wale waliojiita rafiki zake … kuliko vyote. Wewe na mimi, tukiteswa, tuna tabia ya kujitenga na Neno la Mungu; tunataka kutenda visivyo na kupuuza amri zake.
Lakini kutunza au kutathmini kitu kama hazina … ni jambo la maana sana na kama Ayubu, ndivyo vinatupasa kuthamini Neno la Mungu.
Nimeyatunza maneno ya kinywa chake zaidi ya riziki yangu.
Mtazamo huo ndio uliomfanya Ayubu aweze kustahimili mateso.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.