... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kurudishiwa Kipindi Kizuri

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yoeli 2:25-27 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu. Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe. Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe.

Listen to the radio broadcast of

Kurudishiwa Kipindi Kizuri

Download audio file

tunapopambana na vipindi vigumu, tunapoona maishani mwetu matokeo ya dhambi zetu, ni rahisi kufikiri kwamba Mungu anafurahia namna  tunavyosumbuka.  Lakini hii si kweli hata kidogo.

Wazo linatafsiriwa kutoka kwenye neno la Kijerumani schadenfreude – yaani furaha ya kuona mtu anapewa matokeo anayostahili kwa maovu aliyoyatenda – nadhani ni kitu sisi sote tumepitia.  Anastahili adhabu hiyo!  Si kweli?  Lakini wazo hilo kamwe halijaingia kwenye mawazo ya Mungu. 

kama tulivyoona jana, hata kama ataleta matokeo ya dhambi zetu juu ya maisha yetu, moyo wake daima unatafuta ukombozi.  Anataka kutukumbatia tena.  Anataka kutubariki tena kwa upendo wake, kama vile baba mzazi mwema anavyoweza kufanya. 

Hili ni lengo lenyewe analokusudia kwaajili ya watu wake akiwaambia kupitia nabii Yoeli: 

Yoeli 2:25-27 Nami nitawarudishia hiyo miaka iliyoliwa na nzige, na parare, na madumadu, na tunutu, jeshi langu kubwa nililotuma kati yenu.  Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.  Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe. 

Rafiki yangu, nisikilize.  Ikiwa wewe, kwa sababu ya dhambi zako, umeenda mbali na Mungu;  au umejikuta kwenye hatari, basi leo Mungu anaongea na wewe kuhusu upendo wake wa ukombozi.  Leo hii, Mungu anakuita urudi kwake. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.

We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly