... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mafuta ya Roho

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yoeli 2:28,29 Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.

Listen to the radio broadcast of

Mafuta ya Roho


Download audio file

Sijui kama umewhai kuchomwa na jua?  Nakumbuka nilipokuwa mtoto, ngozi yangu ya kizungu ilichomwa vibaya sana. Halafu mama alimimina mafuta ya mizeituni juu ya ngozi yangu kupoza maumivu.  Kusema ukweli, mafuta yale yalikuwa tiba nzuri.

Hivi karibuni tumefuatana na Israeli kipindi walipoadhibiwa kwasababu ya dhambi zao. Mungu alituma nzige na njaa kali juu ya nchi yao. Yaani ilikuwa hatari kabisa. Lakini makusudi ya Mungu kwenye mateso yetu daima – daima! ni kuleta ukombozi. 

Kwahiyo, kupitia nabii Yoeli, alitabiri majira yenye baraka yatakayokuja, kama watu wake wangemrudia. 

Yoeli 2:26-27  Nanyi mtakula chakula tele na kushiba, na kulihimidi jina la BWANA, Mungu wenu, aliyewatendea mambo ya ajabu; na watu wangu hawatatahayari kamwe.  Nanyi mtajua ya kuwa mimi ni katikati ya Israeli, na ya kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu, wala hakuna mwingine; na watu wangu hawatatahayari kamwe. 

Lakini si hayo tu.  Kuna mengine mengi.  Kwasababu kulikuwa na baraka izidiyo Mungu aliyoiandaa kwaajili ya watu wake … baraka ambayo bado ameiandaa kwa watu wake hadi leo:

Yoeli 2:28,29  Hata itakuwa, baada ya hayo, ya kwamba nitamimina roho yangu juu ya wote wenye mwili; na wana wenu, waume kwa wake, watatabiri, wazee wenu wataota ndoto, na vijana wenu wataona maono; tena juu ya watumishi wenu, wanaume kwa wanawake, katika siku zile, nitamimina roho yangu.  

Rafiki yangu, nisikilize! tunapokata shauri na kutubu dhambi zetu, tunamrudia Mungu kutoka moyoni, yeye atamimina Roho yake juu yetu kama vile mafuta ya kupoza – hata juu ya walio wadogo kuliko wote. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy

Make your gift monthly to share more Living Hope!

Hearts are open to Jesus at Easter. Your monthly support will help reach millions around the world to share the hope of Christ.

Make it Monthly