Kusema na Kusikia
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 1:19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika.
Juzi, nilikuwa naongea na rafiki yangu wa karibu anayeishi Canada. Jina lake ni Bob Beasly na tulitumia mawasiliano ya video ya intaneti. Yeye alisisitiza kwamba, majadiliano ya kistaarabu kati ya watu wenye misimamo tofauti hayapo tena, ni kama watu siku hizi hawaheshimiani tena.
Hata mimi ninakubaliana naye. Siku hizi ni kama lengo nikuhakikisha maoni yako yashinde tu, yaani mfumo wa imani yangu ushinde wako. Si kwamba mihadhara imekuwa na uhasama tu, lakini imefikia mahala pia, ukatili unaosababisha sisi (ambao kama Wakristo tunajua vema kwamba msimamo wetu ni sahihi!!) tunazidi kupiga kelele au tunaweza kukimbia na kunyamaza kimya.
Lakini kufanya hivyo, yaani kubishana au kunyamaza sio muitikio mzuri kwa mtu anayekiri kwamba anamuamini Yesu. Haifai kwa mtu anayetaka kufuata nyayo zake na kushirikisha wengine upendo wake katika ulimwengu uliopotea na kuumia.
Sikiliza andiko ninalopenda kulirudia ili iniongozee kujua namna inavyonipasa kuwa na mahusiano na watu tusiokubaliana.
Yakobo 1:19 Hayo mnajua, ndugu zangu wapenzi. Basi kila mtu na awe mwepesi wa kusikia, bali si mwepesi wa kusema; wala kukasirika.
Napenda sana namna Yakobo alivyoorodhesha mambo. Kuwa mwepesi kusikia na si mwepesi wa kusema wala kukasirika. Kuna mwandishi fulani aliongeza hili kwa kufafanua mstari huo:
Wasikilize wengine kwa jinsi wao wanavyopenda kusema, Sema nao kwa jinsi wanavyopenda kusikia.
Kwa maneno mengine, ni kujaribu kuwaelewa wengine na kuwa na majadiliano ya upendo na ustaarabu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.