... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kusudi Kubwa la Mungu

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mwanzo 2:24 Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Listen to the radio broadcast of

Kusudi Kubwa la Mungu


Download audio file

Mara nyingi tunawachukulia wanafamilia kikawaida tu.  Wengi wetu tumekulia katika familia. Wengi tumeanza kujenga familia zetu. Lakini kuna wakati mambo hayaendi kama tulivyotazamia, si kweli?

Familia iliyo bora ni baba na mama wanaofurahi na kupendana, yaani wazazi wakiwa na watoto wengi wanaofurahi, wenye afya njema, wenye maadili mema. Hii ni picha nzuri tunayoijenga katika fikra zetu, sindiyo?  Lakini hali halisi kwa ndugu wengi, au tusema karibu wote, ni tofauti kabisa.

Watu wengi mno, vijana kwa wazee, wanaumia sana kwa sababu ya mahusiano mabaya katika familia au hata kuyakosa kabisa. Kwahiyo turudi nyuma kidogo. Mungu aliumba mwanadamu, mwanamume na mwanamke, ili tuweze kuwa hatimaye … familia.

Mwanzo 2:24  Kwa hiyo mwanamume atamwacha baba yake na mama yake naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.

Ni kweli, si kila mtu anaoa au anaolewa … na tutajadili swala hilo la kubaki bila kuoa au kuolewa siku nyingine. Lakini wengi wanafunga ndoa na ni rahisi kusahau kusudi kubwa la Mungu. Kwamba mwanamume anaacha wazazi wake na anaambatana na mke wake. Wawili wanakuwa mmoja – kimwili, kihisia, kiroho.  Mwanamume huyu na mwanamke huyu, watu wawili tofauti, wanakuwa mmoja. Hapo ndipo kuna msingi wa ujamaa na familia.  Huu ndio mpango wa Mungu; ni kusudi lake kubwa sana.

Wawili … kuwa mmoja.

Kwahiyo kama wewe ni mme au wewe ni mke, je!, Ninaweza kukuuliza kama wewe na mwenzi wako, mko wawili au mko mmoja?  Uwe muwazi.  Kwa sababu kama kweli bado mko wawili … basi ni dhahiri kwamba familia yako tayari imeanza kusambaratika.

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy