Kutamani Mambo ya Duniani
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 2:15,16 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Unafiki ni tabia mbaya mno tena ya hatari kama tukiiruhusu kuingia ndani ya maisha yetu – hususani pale wanaodanganywa ni sisi wenyewe! Tunakiri kwamba tunamwamini Yesu lakini tunaishi kama hatumwanini.
Sisi sote tunapenda kuitazama Injili ya Kristo kupitia mitazamo inayotokana na hali halisi ya mazingira tunayoishi. Mtu akiishi kwenye nchi tajiri, kama mimi, ataitazama Injili kwa mtazamo wa tajiri. Wanaoishi kwenye hali duni wanaitazama kwa mtazamo wa umaskini wao pamoja na matamanio waliyo nayo. Wanaosetwa nao wataitazama Injili kwa mtazamo wa shauku ya kuwekwa huru, n.k …
Kitu ninachotaka kukisema hapa ni kwamba, katikati ya hali halisi ya mazingira yetu, hatimaye tunaweza kuanza kutamani mambo ya dunia kuliko tunavyotazamia kuona Ufalme wa Mungu unapanuka na namna utawala wa Kristo unavyozidi kubadilisha mitazamo yetu na tabia zetu. Huu ndio ukweli wa mambo. Kwahiyo tujikague tena:
1 Yohana 2:15,16 Msiipende dunia, wala mambo yaliyomo katika dunia. Mtu akiipenda dunia, kumpenda Baba hakumo ndani yake. Maana kila kilichomo duniani, yaani, tamaa ya mwili, na tamaa ya macho, na kiburi cha uzima, havitokani na Baba, bali vyatokana na dunia.
Hayo ni marekebisho makubwa ya mwelekeo wa mtu kuliko yote nimewahi kuyasikia. Je! Wewe unaiangalia Injili ya toba na msamaha kwa mtazamo upi? Je!, ni Tamaa ya mambo ya dunia na matamanio yako yanakuzuia kwa kiwango cha kukuzuia usibadilishwe kuwa mtu mwema, mpole, mnyenyekevu na mkarimu – kama vile Yesu anavyotaka uwe?
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.