... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Mwisho wa Dunia

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Yohana 2:17 Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele.

Listen to the radio broadcast of

Mwisho wa Dunia


Download audio file

 Siku moja mambo yote tunayothamini duniani – mahusiano yetu, mali zetu na hata sifa tulizo nazo – vyote vitapita.  Yaani yale yote tunayoyafanya kama kipaumbele hayatakuwa na maana tena.

Ni dhana inayomfanya mtu kutafakari hasa katika ulimwengu huu unaotuahidi mambo mengi, labda ni muda mwafaka wa kuwa makini.  Si vibaya kuweka kipaumbele kwa familia yako pamoja na shughuli zako na mengine mema, lakini siku moja yote yatatoweka. 

Sasa tunajikuta tunaishi katika uchaguzi mwingi mno unaoleta hatari yakutuzubaisha tusilenge mambo muhimu zaidi, yaani ukweli wa uwepo wa Mungu mwenyewe. 

Je!, Utaniruhusu nikikuulize kama kidogo-kidogo, unazidi kulenga muda huu wa sasa na mambo yatakayopita kuliko kumlenga Mungu wetu aliyemtuma Yesu afe ili uwekwe huru na hayo yote na kufufuka tena akuletee maisha mapya ya uzima wa milele?  Nilikuwa ninauliza tu kwa sababu … 

1 Yohana 2:17  Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. 

Maisha yetu ya hapa duniani ni kama chembe ya mchanga tu katika ulimwengu mzima kwasababu maisha tutakaoishi itaendelea upande wa pili wa kaburi, na kuendelea milele daima.  Maisha hiyo haitakuwa na mwisho.  Na maisha hiyo mtu ataiishia ama mbele za Mungu ama katika mateso, akitengwa naye.  

Na dunia inapita, pamoja na tamaa zake, bali yeye afanyaye mapenzi ya Mungu adumu hata milele. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.