Kutangaza Neema
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Luka 2:10-12 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.
Wakati mtu anakutendea mema ambayo hukustahili, yaani hukustahili hata kidogo, ni vigumu kuyaelewa kwa haraka. Hua inachukua muda kuipokea kama ilivyo, si kweli? Ndivyo ilivyokuwa Krismas ile ya kwanza.
Ebu jaribu kufikiria kana kwamba uliishi karne ile ya kwanza huko Israeli. Bila shaka wewe ni mlala hoi, isitoshe, Warumi walikuwa wameivamia nchi yako na viongozi wenu wa dini ambao wangewatetea na kuwajali wako wanatafuta maslahi yao wenyewe binafsi tu – mara nyingi wakishirikiana na Mkoloni Mrumi.
Wewe ulikuwa Myahudi, anayeishi chini ya sheria ya Mungu, yaani Torati kama wanavyosema, ila hukuishika kikamilifu. Yaani usingeweza kuishika kikamilifu. Hata kusema umeivunja ni mara nyingi. Bila wewe kujua, Mungu alikuwa anakamilisha mpango wake kwa ajili ya ulimwengu huu. Mpango wa neema. Mpango wa rehema. Mpango wake wa wokovu kwa ajili yako. Ni mpango uliokuwa umeandaliwa tangu zamani.
Anaingiaje ulimwenguni humu? Anatangazaje kusudi lake? Kwa kutumia utukufu wake kuwaang’aria usiku ule, kutangazia kusudi lake kwa wachungaji waliokuwa wanalinda kundi lao.
Luka 2:10-12 Malaika akawaambia, Msiogope; kwa kuwa mimi ninawaletea habari njema ya furaha kuu itakayokuwa kwa watu wote; maana leo katika mji wa Daudi amezaliwa kwa ajili yenu, Mwokozi, ndiye Kristo Bwana. Na hii ndiyo ishara kwenu; mtamkuta mtoto mchanga amevikwa nguo za kitoto, amelala katika hori ya kulia ng’ombe.
Mungu anafanyaje ili akutangazie kule kondeni habari ya mpango wake wa wokovu? Kwa kukwambia wewe mchungaji, kwamba utamkuta wapi? Kwenye hori ya kulio ng’ombe, akivikwa nguo za kitoto. Ndivyo Mungu alivyotangaza neema yake kwako, siku ile ya kwanza ya Krismas.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.