... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Neema Iliyochafuliwa

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Luka 2:7 Akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni.

Aaah, tumefika tena majira ya Krismasi!  Kwa wengine ni wakati wa pirika-pirika, wengine ni kipindi cha upweke.  Ningependa kujua unachofikiria unapotafakari habari za Krismas.

Juzi asubuhi nilikuwa naomba nikimshukuru Mungu kwamba kabla ya kuumba chochote alinichagua nifaidike na neema yake. nikichunguza nilivyoishi zamani, niligundua tena kwamba sistahili, Lakini hii ndiyo maana ya neema.  Neema ya Mungu ni bure tena hakuna astahiliye, lakini tunaipokea kwa sababu alimtuma Yesu ulimwenguni. 

Nilikuwa nimemwasi Mungu, Nilivunja amri zote, Lakini kama vile mtu fulani alivyosema, neema inachora picha nzuri bila kuangalia masharti ya dini.  Ni amina kubwa sindiyo?  Neema ya Mungu inatufikia katika ulimwengu wetu uliochafuka mno, katika maisha yetu yaliyochafuka bila kuangalia “kanuni za dini”.  Na hapo ndipo habari hii ya neema ilipoanzia – Mwokozi kukubali kuingia katika machafuko. 

Luka 2:7  Akamzaa mwanawe, kifungua mimba, akamvika nguo za kitoto, akamlaza katika hori ya kulia ng’ombe, kwa sababu hawakupata nafasi katika nyumba ya wageni. 

Hakuzaliwa katika jumba la kifalme bali kwenye sehemu ya kuchunga mifugo.  Hakuzaliwa ndani ya kitanda bali katika hori ya kulia ng’ombe. Je! Umewahi kusogelea ng’ombe?  Wana harufu mbaya.  Wanachafua mazingira.  Mate yao yanatoka, kinyesi  na majani yamejaa kwenye mazizi yao. 

Yaana, kuzaliwa kwa Mwokozi wetu Yesu hakukuwa ndani ya hospitali safi.  Ni kama hakukuwa na mpangilio wowote.  Mazingira hayakumfaa Mfalme wa wafalme aliye Bwana wa mabwana, muumba wa mbingu na nchi.  Ni kama alichafuliwa.  Lakini daima neema haijali hayo.  Yesu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.