Kutazamia Mwisho wa Mambo Yote
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 1:6 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.
Tazama! Wiki ya kwanza ya mwaka mpya inakaribia kuisha. Ukiendelea katika wiki ya pili, ya tatu, ya nne, je! Una mipango gani? Swali lingine lililo muhimu zaidi, je! Unadhani ni mpango upi Mungu anao kwa ajili ya maisha yako?
Ni swali linalovutia. Tunaweza kushughulishwa sana na matazamio yetu na ndoto zetu mpaka tusiwaze hata kidogo kwamba Mungu anayo matazamio na ndoto kwa ajili ya maisha yetu pia. Ni mzazi yupi asiyekuwa na matazamio kwa watoto wake?
Kwa hiyo, baada ya kukuita akukumbatie katika mikono yake ya upendo, baada ya kukusamehe kupitia kifo cha Yesu pale msalabani, baada ya kukukirimia maisha mapya na uzima wa milele kupitia ufufuo wake kutoka kaburi lile lililo wazi sasa … ni matumaini gani, ni ndoto gani, ni mipango gani Mungu anayo kwa ajili yako? Hivi ndivyo Mtume Paulo aliandikia rafiki zake pale Filipi:
Wafilipi 1:6 Nami niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hata siku ya Kristo Yesu.
Kwa kweli Mungu ameshaanza kazi njema moyoni mwako kwa kukuita na kukukaribisha kwake kupitia imani yako ndani ya Yesu, kwa kukuosha dhambi zako, kwa kukujaza Roho wake Mtakatifu ambaye ni uwepo wake halisi ndani yako.
Mpango wake sasa ni upi? Ni kuikamilisha kazi ile ya ajabu. Kuendelea kukunyonsha, kukukuza, kukuvuta karibu zaidi kupitia milima na mabonde aliyepanga kwa ajili ya maisha yako. Kutimiza kazi yake njema na kubwa ndani yako hadi utakapofurahia kuwepo mbele zake milele na milele.
Kwa hiyo, usizubaishwe. Kaza macho kule mbeleni kwa mwisho wa mambo yote.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.