Kutegemezwa na Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wafilipi 4:11-13 Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Maandiko Matakatifu huwa yanatumiwa vibaya, kuna mstari mmoja huwa unatumiwa sana, “Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.” Watu wanayatumia maneno hayo kwa kutaja na kudai vitu vingi mbalimbali. Lakini sio lengo la mstari huo. Sio tafsiri yake.
Namkumbuka mtu mmoja aliyetumia mstari huo akimdai Mungu ampe gari la kifahari lenye bei kubwa. Wengine wanautumia kwa matamanio yao ya mafanikio. Ni kama wanabadilisha mstari huo useme hivi: Yesu atanisaidia kufaulu katika jambo lolote natakalo kulifanya.
ebu tuchunguze tena maandiko hayo:
Wafilipi 4:11-13 Si kwamba nasema haya kwa kuwa nina mahitaji; maana nimejifunza kuwa radhi na hali yo yote niliyo nayo. Najua kudhiliwa, tena najua kufanikiwa; katika hali yo yote, na katika mambo yo yote, nimefundishwa kushiba na kuona njaa, kuwa na vingi na kupungukiwa. Nayaweza mambo yote katika yeye anitiaye nguvu.
Tujaribu kumuelewa Mtume Paulo wakati alipokuwa anaandika maneno hayo, alikuwa amefunga jela akisubiri hukumu ya kifo. Anachokisema ni hiki, kwamba haijalishi Mungu amemwagiza afanye nini, ikiwa jambo rahisi au gumu, Yesu atamsaidia kuitimiza. Billy Graham alisema hivi, Mapenzi ya Mungu hayatakupeleka mahali ambapo neema yake isingeweza kukutegemeza.
Kumbuka kwamba Kristo ndiye awezaye kukupa nguvu ya kutimiza yale ameyokwambia uyafanye.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.