... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kuthubutu Kujihatarisha kwa Imani

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Mathayo 6:6 Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.

Listen to the radio broadcast of

Kuthubutu Kujihatarisha kwa Imani


Download audio file

Mimi binafsi naona kama dini, au kuwa mfia fidi ni zoezi bandia tu.  Mtu anapitia mazoezi yote, lakini mwishowe, haizai chochote.  Sijui kama umeshashuhudia hayo?

Tunachokitaka sisi sote, kama kweli tutakuwa na mahusiano na Mungu, ni kuwa na kitu halisi, chenye maana, kitu kinachoweza kuleta msaada katika kipindi kigumu. 

Hivi karibuni nimepokea barua pepe kutoka kwa rafiki wangu mpendwa, Lowell Wertz, mishionari anayetumika barani Afrika kwa zaidi ya miaka 40.  Aliandika hivi: 

“Ninataka kukushirikisha matukio mawili pale ambapo Mungu alidai imani kwangu.  Furaha katika Mavuno (huduma anayoiongoza) tulikuwa na dola $3,000 kwenye akaunti ya benki wakati tunaingia nchini Tanzania.  Baada ya wiki chache, maelfu ya wakimbizi wenye njaa waliingia Mkoa wa Kigoma.  Nilifahamu kile ambacho Mungu alitaka tufanye. Kwa imani tulitumia pesa zetu zote kununua chakula kwa ajili ya wakimbizi. Daima mtu atakuwa na hofu pale anapothubutu kuhatarisha maisha yake kwa kutumia imani yake.  Lakini hata hivyo, ndani yake, atakuwa na uhakika kwamba jambo jema linaenda kutendeka. Imani yangu ilikua na niliamini kwamba Mungu anaweza kukidhi mahitaji yetu yote.  Mungu anataka  mahusiano yetu nayeye na imani zetu ndani yake ziwe halisi kabisa.” 

Hapo ndipo kuna jibu. Tunataka mahusiano yetu na Mungu yawe ya kweli lakini hii inawezekana tu pale imani yetu inakuwa halisi bila unafiki.  Kwa hiyo … 

Mathayo 6:6  Bali wewe usalipo, ingia katika chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele za Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi. 

Ukithubutu kutumia imani hatarini, lazima uondoe unafiki pia. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.


We use cookies to improve your browsing experience, analyse site traffic & personalise content, but we do not track you when you leave this site. To find out how we utilise & protect your data, check out our "Privacy Policy".

Privacy Policy