... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Tayari Amedhibiti Kila Jambo

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Wakolosai 3:15 Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani.

Listen to the radio broadcast of

Tayari Amedhibiti Kila Jambo


Download audio file

Tunaposhindwa kudhibiti hisia zetu – hasira, hofu, kujiona kwamba hatufai chochote kile– zinatunyima amani ya Mungu.  Sasa tukikosa amani, tutajikuta hatarini kwa sababu ni kama tunajianda kupigana na watu wengine.

Sasa ungechagua nini, amani au mapigano endelevu?  Nadhani jibu ni rahisi, sindiyo?  Sisi sote tunatamani kuwa na amani na kutokuwa tena na mapambano maishani. 

Ukisoma ndani ya Biblia, utagundua kwamba, amani ni jambo muhimu sana machoni pa Mungu.  Ni baraka ambayo anawabariki watu wake kwayo walipomheshimu wakati wa Agano la Kale. 

Pia, Yesu aliwaahidia wanafunzi wake amani katika siku zile za hatari akikaribia kusulubiwa. Amani ni ahadi ya Mungu ndani ya Agano Jipya kwa wale wanaomwamini Yesu.  Lakini kupokea amani yake ni hiari yetu sisi wenyewe. 

Wakolosai 3:15  Na amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu; ndiyo mliyoitiwa katika mwili mmoja; tena iweni watu wa shukrani. 

Ebu tufikirie kidogo.  Tunaweza kuamua kuruhusu amani ya Kristo kutawala mawazo yetu au la.  Tukikataa – na sisi sote tumewahi kuamua hivyo – matokeo si mazuri, Tukiwa wachokozi, tutaamua vibaya na kujiletea matokeo mabaya mno.  Maisha huwa yamejaa migogoro na hali hiyo inachosha kabisa, inaumiza na nadhani kwamba hakuna anayeitaka hata kidogo.

Lakini tukiruhusu amani ya Kristo kuongoza mawazo yetu … itatuletea amani.  Tena ukitafakari kidogo, utaona kwamba amani na kuishi maisha ya ushindi vinaenda sambamba.  Amani ya Kristo iamue mioyoni mwenu.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.