Kutilia Mashaka Neno la Mungu
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mwanzo 3:1-5 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Siku hizi ni rahisi sana kushawishika na kuanza kutilia mashaka Neno la Mungu; kufuta mistari inayotukera na kutusumbua ndani ya Biblia ili iweze kupendeza zaidi na kwenda sambamba na maisha yetu ya karne hii ya ishirini na moja.
Je! Ni kweli Mungu hapendezwi na mwanamume au mwanamke kuishi pamoja nje ya ndoa?, Je!, Jehanamu ni mahali pa mateso milele? Hii haiwezikani!, Je Shetani yupo kweli kweli? Acha bwana, ni hadithi za kizee tu!
Ndivyo watu wengi wanavyojiita kwa jina la Kristo wanafikiri. Na mawazo kama hayo yanamomonyoa nguvu ya Neno la Mungu maishani mwao. Lakini hili si jambo jipya hata:
Mwanzo 3:1-5 Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya BWANA Mungu. Akamwambia mwanamke, Ati! Hivi ndivyo alivyosema Mungu, Msile matunda ya miti yote ya bustani? Mwanamke akamwambia nyoka, Matunda ya miti ya bustanini twaweza kula; lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema, Msiyale wala msiyaguse msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa kama Mungu, mkijua mema na mabaya.
Unaona? Adui hakujaribu kuwashawishi Adamu na Hawa waue, au waibe au waseme uongo. Aliwashawishi waanze kutilia mashaka Neno la Mungu. Hatari ilianzia hapo hapo
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.