Kama Mfu … Lakini Mungu!
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Waebrania 11:11,12 Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.
Kuna wakati Mungu anatupeleka mahali pasipowezekana, tukae pale kwa kipindi fulani katika “hali ya imani hatarishi”. Sasa mtu atastahimili mpaka lini? Ni lini itampasa kuamka na kukabiliana na hali halisi ya mambo?
Mtu yeyote aliyeanza safari ya imani basi atakuwa ameshawahi kujiuliza, “kweli Mungu yuko pamoja nami kwenye safari hii, au niliibuni mimi mwenyewe kwenye fikra zangu tu?” Hiki ni kitendawili cha imani, Angalia mfano wa Ibrahimu na Sara. Hawakuweza kuzaa watoto, na Mungu alipowaahidi kuwa na mtoto, tayari walikuwa wameshapitwa na wakati, yaani wazee.
Waebrania 11:11,12 Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu. Na kwa ajili ya hayo wakazaliwa na mtu mmoja, naye alikuwa kama mfu, watu wengi kama nyota za mbinguni wingi wao, na kama mchanga ulio ufuoni, usioweza kuhesabika.
Sasa walipohama nchi yao na kuacha maisha ya starehe na kuanza safari isiyoeleweka, tayari walikuwa na umri wa miaka sabini na tano. Ndipo Mungu alipowaahidi uzao. Lakini ilikuwa baada ya miaka mingine ishirini na tano, yaani wakati wanatimiza umri wa miaka mia moja (!!) ndipo Mungu anawapa mtoto, Isaka, kutoka kwenye miili yao iliyokuwa kama iliishakufa.
Nisikilize, kama una uhakika kwamba ulichokipata kimetoka kwa MUngu, (hata kama kina yumba-yumba, au kinaonekana kimekufa) ujue kwamba bado hakijafaa!
Kwasababu Mungu ana mpango, kamwe hauwezi kufa bure hadi atakapoutimiza.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.