... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kutoka Hema Hadi Mji

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Waebrania 11:9,10 Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile. Maana alikuwa akiutazamia mji wenye msingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu.

Listen to the radio broadcast of

Kutoka Hema Hadi Mji


Download audio file

Kuna kosa kubwa tunalolifanya wewe na mimi, ni kufikiri kwamba mipango ya Mungu inatulenga sisi na starehe zetu na manufaa yetu tu. Ni kosa kubwa kwa sababu mipango yake ni mikubwa sana kuliko yetu sisi.

Miezi iliyopita, nilikuwa ninaongea na rafiki yangu ambaye ni mkulima, na mashamba yake yaligharikishwa na mafuriko makubwa kupita yote yaliyokumbwa. Tuliongelea siku mafuriko yalipofikia kilele na akaniambia kwa mtazamo wake kwamba ni kosa kumwomba Mungu azuie mafuriko badala ya kumwomba mapenzi yake yaonekane na atuwezeshe kutenda mema yote aliyokusudia tuyafanye katika mazingira yale. 

Yaani ni oni la imani yenye nguvu alilotoa wakati ule. Kumbe, alikuwa anasaidia jirani yake aliyegharikishwa na maji akiwa na ng’ombe 600 kwa kuwakamua mara mbili kwa siku. Pia, alikuwa anasaidia vikosi vya dharura waliofika mahali pale, akiwaazima vifaa mbalimbali. Isitoshe, alitumia mtumbwi wake asubuhi mapema siku ya Krismasi kwenda kumchukua mchungaji upande wa pili wa mto ili waamini waweze kuendelea na ibada siku ile ya Krismasi. 

Kuna mfano wa Ibrahimu pia: 

Waebrania 11:9,10  Kwa imani alikaa ugenini katika ile nchi ya ahadi, kama katika nchi isiyo yake, akikaa katika hema pamoja na Isaka na Yakobo, warithi pamoja naye wa ahadi ile ile.  Maana alikuwa akiutazamia mji wenye msingi, ambao mwenye kuubuni na kuujenga ni Mungu. 

Ibrahimu alianza safari ya mashaka isiyo na starehe kwa muda wa miaka ishirini na mitano katika Nchi ya Ahadi lakini hakuweza kuona namna mji wa Yerusalemu ulivyojengwa pale baada ya karne nyingi baada yake. 

Lakujikumbusha:  Mipango ya Mungu haikulengi wewe peke yako. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.