Kuwa na Mtazamo Tofauti
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Matendo 15:37-39 Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao. Bali Paulo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfilia, asiende nao kazini. Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kipro.
Bado ninashangaa kuona namna watu wawili wanaweza kuchunguza ishu moja, kitu kimoja lakini mitazamo miwili tofauti kabisa. Kwanini huwa inatokea hivyo? Inakuwaje?
Nilihudhuria kongamano siku za hivi karibuni hizi na kuna mwanamke aliketi karibu yangu, kumbe alikuwa na simu janja kama hii ya kwangu kabisa. Tuliziweka mezani, skrini zikiwa chini.
Simu yangu ilikuwa na kava ya bluu, ila niliishangaa simu ya yule mwanamke, ilikuwa na kava angavu lakini alikuwa ameibandikia picha ndogo ndogo nyingi kwa ajili ya kuifunika ile kava. Jamani!, Mimi nisingeweza kuivumilia kava hiyo, ingenichanganya kabisa!
Simu mbili zacaina moja, mali za watu wawili tofauti, wakiwa na mitazamo tofauti. Maisha, ndivyo yalivyo. Lakini haya si mapya.
Matendo 15:37-39 Barnaba akaazimu kumchukua Yohana aliyeitwa Marko pamoja nao. Bali Paulo hakuona vema kumchukua huyo aliyewaacha huko Pamfilia, asiende nao kazini. Basi palitokea mashindano baina yao hata wakatengana. Barnaba akamchukua Marko akatweka kwenda Kipro.
Hawa mashujaa wawili ndani ya Biblia – Paulo na Barnaba – Mungu aliwatumia kutenda makuu. Lakini walikuwa bado wenye dhambi kama wewe na mimi. Kule kutofautiana kwao kulisababisha mashindano kati yao.
Binadamu daima – nisikilize vizuri, daima! – watakuwa na mitazamo tofauti tofauti. Lakini isisababishe mabishano. Tunaweza kukubali kwamba tunaweza kutofautiana, lakini ifanyike katika upendo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.