Kuwa na Nguvu Zaidi
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Yakobo 5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa.
Lazima ukubali kwamba hata kama wewe ni mtu mwenye nguvu, bado sisi sote tunajisikia kuwa wanyonge – tukikosa nguvu ya kupambana na mambo maishani mwetu.
Bila shaka hata wewe umewahi kujisikia kwamba umeshindwa kukabiliana na changamoto, ikiwa katika mazingira yako au ukiwa ndani ya mawazo yako au hisia zako.
Kama wewe ni mwenye busara utamwomba Mungu utaomba na kuomba lakini hakuna jibu, ikiwa hivyo utafanyaje? Acha nikujibu kwa kukuuliza swali lingine. Je ukiwa unaomba huwa unaombaje? Nataka kusema hivi, Ukikaribia kiti cha neema, unaamini kupata nini?
Yakobo 5:16 Ungameni dhambi zenu ninyi kwa ninyi, na kuombeana, mpate kuponywa. Kuomba kwake mwenye haki kwafaa sana, akiomba kwa bidii.
Mstari huu unaonekana katika masimulizi yanayohusu kuombea wagonjwa ili waponywe. Lakini kuna mambo mawili nataka uelewe. Kwanza, habari ya kukiri dhambi zako, Ni kwa sababu dhambi ina tabia mbaya ya kuzuia majibu ambayo Mungu angetujibu.
Pili, tukimwendea Mungu tukiwa tumesamehewa, tukiwa tumeoshwa, tukiwa safi, na “kuhesabiwa haki” kwa imani yetu ndani ya Yesu, basi maombi yetu yatafaa sana na kuwa na nguvu!
Je! Unaamini hayo? Inabidi uamini. Ni kweli kabisa.
Angalia, Mungu hatatujibu maombi yetu kila mara kwa wakati sisi tunataka wala kwa njia tunaotazamia, lakini ukiishi maisha inayojaa maombi, utaishi maisha inayojaa uwezo.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.