... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Kupanda na Kushuka

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

Yakobo 5:13 Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.

Listen to the radio broadcast of

Kupanda na Kushuka


Download audio file

Sijui wewe unawaza nini, lakini mpango nilio nao kwa ajili ya maisha yangu ni kwamba niendelee shwari tu, nikiwa na siku kadhaa za kuchangamka zaidi, Je!  Unaonaje, si mpango mzuri? 

Lakini ni dhairi kwamba sivyo maisha ilivyo.  Tunakutana na milima na mabonde, matatizo yanaweza kutujia ghafla. Lakini hata hivi, inawezeka  kitu kikatokea ghafla ambacho kinamshusha mtu au kinamwinua.  Maisha ndivyo ilivyo. 

Ikiwa unamwamini Yesu na kupata shauku ya kumheshimu na kumtii, basi yu pamoja na wewe popote ulipo hata kama maisha yabadilikeje.  Sikiliza Neno linaloeleza jinsi ya kukabiliana na kule kupanda na kushuka: 

Yakobo 5:13  Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya?  Na aombe.  Ana moyo wa kuchangamka?  Na aimbe zaburi. 

Maneno machache mno lakini matamu yenye nguvu.  Hatuna budi kupatwa na mabaya, basi uwe na juhudi katika kuomba.  Yakikujia umwendee Mungu mara moja, si penginepo.  Matatizo yakija, jua ya kwamba yuko pamoja na wewe pale pale.

Halafu ukipata siku za Baraka, siku za furaha, basi imba, changamka, ufurahi; ukimsifu Mungu kwa ajili ya wema wake; ukimshukuru kwa ajili ya baraka zake.  Mimi nadhani kuna muda hatusherehekee vipindi vizuri kama inavyotupasa – tusisahau kwamba hapo napo Mungu yupo pia anastahili kuhimidiwa kabisa! 

Mtu wa kwenu amepatikana na mabaya?  Na aombe.  Ana moyo wa kuchangamka?  Na aimbe zaburi.  

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.