Kuwa Sahihi na Kuwa Mwenye Fadhii
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Mithali 21:21 Aandamaye haki na fadhili, ataona uhai na haki na heshima.
Nadhani unafahamu inavyovunja moyo pale unapojua uhakika ya kwamba wewe uko sahihi lakini kuna mkorofi (samahani, lakini ndivyo mpinzani wako anavyoonekana, si kweli?!) akizidi kubisha akiwa na jazba pia.
Na tukisema ukweli, kwa asili ya kibinadamu, unaweza kutaka kumpiga ngumi; si kweli?! inakatisha tamaa kweli kweli, Au tutoe mfano mwingine usio mkali sana. Tuseme uko kazini na mfanyakazi mwenzako au mtu wa chini yako anaanza kufanya kosa kwenye kazi yake. Kwahiyo mara moja unamkandamiza kwa kumkemea kwa kutengeneza kosa lake bila kujali anavyojisikia yeye.
Ninachotaka kusema ni kwamba, mara nyingi tukiamua kati ya kuwa sahihi na kuwa mwenye fadhili ni uchaguzi sahihi. Fadhili?.. hivi fadhili ni muhimu kweli?
Mithali 21:21 Aandamaye haki na fadhili, ataona uhai na haki na heshima.
Ni kweli, hapa tumesoma habari ya “haki”, si swala la “usahihi” lakini hata hivyo ni kama kitu kimoja … au vinategemeana. Kama unawaza “kuwa sahihi” basi ni sawa na kutenda haki, vinafanana.
Lakini ukifikiri kwamba “kuwa sahihi” ni kupata unachokitaka wewe na kufikia lengo ambalo wewe unaona ni sahihi bila shaka, lakini huko ukimvunjia heshima mwenzako na kukosa kumstahi na kumwonyesha fadhili, ujue kwamba havifanani hata kidogo.
Kwahiyo, ukijikuta mahali ambapo haki na fadhili hazipatani, kwamba ni kuchagua moja na kuacha nyingine, basi ujue kwamba umechagua tafsiri isiyo sahihi ya “kuwa sahihi”.
Aandamaye haki na fadhili, ataona uhai na haki na heshima.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.