... helping you be all that God made you to be, because He plans on shining His light into this world through you.

Berni - ceo, Christianityworks

Shikilia Sana Msalaba

We're glad you like it!

Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.

Register or Login

Add to Favourites

1 Wakorintho 1:18,19 Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa.

Listen to the radio broadcast of

Shikilia Sana Msalaba


Download audio file

Sijui kama umeshawahi kuzalilishwa, kukataliwa na kudhihakiwa kwasababu ya kumuamini Yesu, lakini acha nikwambie, si jambo linalopendeza. Lakini hata hivyo, ukitafakari kidogo si jambo la kushangaza.

Bila kupendelea, hebu tuchunguze neno la msingi la imani ya Kikristo; kwamba sote tumetenda dhambi, kwahiyo hatuwezi kustahili kukubaliwa na Mungu.  Lakini alitupenda kiasi cha kumtuma Yesu kufa msalabani kulipa deni la dhambi zetu, ili amwaminiye yeye aweze kuoshwa machoni pa Mungu na kuishi naye milele mbinguni. 

Lakini kama wewe ni mtu wa kawaida anayepambana na maisha, mtu ambaye hajapata kusikia vizuri habari za Ukristo kwa ujumla … imani hiyo ya msingi ni jambo geni kabisa lakushangaza mno.  Mbona mimi sijawa mbaya sana.  Isitoshe, kama Mungu ananipenda, kwanini asinisamehe tu?  Kwanini kuchukua hatua kali hiyo ya kusababisha Mwanae auawe kwasababu ya makosa yangu? 

1 Wakorintho 1:18,19  Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu.  Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, na akili zao wenye akili nitazikataa. 

Kwakweli, haieleweki kabisa. Ndio maana wengi wanaipinga! Ndio maana watu wanaweza kufikiri kwamba wewe ni mjinga kwa kuiamini. Ndio maana wanakudhalilisha, na kukukataa na kukutukana. 

Lakini kwako wewe, kama kweli unaamini, unaokoka siku baada ya siku kupitia imani yako ndani ya Yesu.  Kwahiyo, ulimwengu unapokupigia kelele na kukuzomea kwamba umerukwa na akili, kuna jambo moja tu la kufanya.  Shikilia msalaba. 

Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.