Laiti …!
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Isaya 48:17,18 BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari.
Kujuta ni hisia ambayo hakuna mtu anayependa kuisikia. Lakini kumbe, tunaifahamu vizuri. Si kwamba tumelisoma neno “majuto” kwenye kamusi, bali ni kwasababu sisi sote tumewahi kujutia kitu fulani tulichokifanya.
Laiti nisingesema hivyo! Laiti nisingefanya hivyo! Laiti nisingekumbuka…. hayo ndio majuto.
Jaribu angalau kufikiria majuto waliyokuwa nayo Waisraeli wakati wamehukumiwa miaka sabini kukaa hali ya wafungwa huko Babeli kwa sababu wamemwacha Mungu na kuabudu sanamu. Kwahiyo Mungu aliwaruhusu Wababeli kubomoa Yerusalemu mpaka misingi … wakateka watu wake na kuwapeleka wawe watumwa wao.
Sasa Mungu alipoanza mipango ya kuwaweka huru na kuwarejesha kwenye Nchi ya Ahadi, ilibidi awakumbushe hivi:
Isaya 48:17,18 BWANA, mkombozi wako, mtakatifu wa Israeli, asema hivi; Mimi ni BWANA, Mungu wako, nikufundishaye ili upate faida, nikuongozaye kwa njia ikupasayo kuifuata. Laiti ungalisikiliza amri zangu! Ndipo amani yako ingalikuwa kama mto wa maji, na haki yako kama mawimbi ya bahari.
Laiti … laiti wangalimtii Mungu. Ndio haya. Ndilo Neno lake la kutuonya leo, mimi na wewe. Katika kutii, kuna baraka, fadhili za Mungu zikikufuata popote tuendapo. Pia, kuna matokeo ya kuasi.
Usijikute tena katika hali hiyo ya majuto, ukisema “Laiti ningali …” Umtii Mungu.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.