Maana Halisi ya Unafiki
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
1 Yohana 4:19-21 Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
Lazima tukubali kwamba kuwapenda watu wengine, kuna wakati kunatuwia vigumu. Wao kuna wakati hawatutendea haki. Kuna wakati hawafanyi kama tulivyotazamia watende. Halafu, kidogo-kidogo … hali hii inakuwa kero.
Bila shaka, kuna watu katika maisha yako leo hii ambao wanakuletea furaha kubwa. Pia, kuna wengine ambao ukikumbuka nyuso zao tu, mara moja hisia zinapanda, hisia za maumivu na hasira.
Labda wamekukosea na kukudhulumu. Labda wamekukwaza kwa njia moja au nyingine. Labda wana mawazo tofauti kabisa ambayo usingeweza kukubaliana nayo. Mwitikio wa kawaida wa kibinadamu dhidi ya watu hawa ni kuanza kufanya moyo wako kuwa mgumu kidogo kidogo ili uweze kujilinda nao.
Shida iliyopo ni kwamba kadiri unapofanya moyo wako kuwa mgumu, ndipo ile hasira iliyopo ndani yako inazidi kukereketa mpaka inakutafuna kabisa. Hapo ndipo Neno la Mungu laweza kuleta tiba kwa hali kama hiyo:
1 Yohana 4:19-21 Sisi twapenda kwa maana yeye alitupenda sisi kwanza. Mtu akisema, Nampenda Mungu, naye anamchukia ndugu yake, ni mwongo; kwa maana asiyempenda ndugu yake ambaye amemwona, hawezi kumpenda Mungu ambaye hakumwona. Na amri hii tumepewa na yeye, ya kwamba yeye ampendaye Mungu, ampende na ndugu yake.
Ebu fikiria kidogo. Unafiki halisi ni kuona Mkristo anayezunguka huku na huko, mistari ya Maandiko midomoni lakini moyoni pamejaa chuki.
Acha Neno la Mungu likuweke huru leo. Umkaribishe Roho Mtakatifu moyoni mwako aweze kuulainsha, na kuuponya na kukuweka huru na chuki.
Sisi twapenda kwa maana Mungu alitupenda sisi kwanza.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.