Maombi Yangu kwa Ajili Yako
We're glad you like it!
Enjoying the content? You can save this to your favorites by logging in to your account.
Wakolosai 1:9-11 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha.
Leo ninataka kukushirikisha jambo ninalolionea shauku kubwa; jambo linalonipa motisha, linalonisukuma kufanya ninachokifanya. Ni hili – kutaka kuona unavyokua na kuwa mtu mzima kwenye mahusiano yako na Yesu, mahusiano yanayopendeza na yenye nguvu.
Mtume Paulo aliandika karibu nusu ya vitabu vya Agano Jipya. “Vitabu” vile vinatujia leo kwa mfumo wa barua zilizoandikiwa makanisa mbali mbali – mengine yalianzishwa nayeye Mwenyewe na wahudumu wenzake. Halafu ndani ya nyaraka zile, hata kama ilibidi mara kwa mara kuwakaripia, mfano kwa Wakorinto na Wagalatia, moyo wake wa uchungaji bado ni dhairi, huwezi kukosa kuuona ukizisoma.
Na mimi pia, nina nia hiyohiyo kwa ajili yako na wengine wote wasiohesabika wanaosikiliza kipindi hiki cha Neno Safi na Lenye Afya, au kukisoma au kukiangalia kwenye televisheni. Kwahiyo, wakati nasoma maneno Paulo aliyowaandikia kanisa la Kolosai, kweli niliguswa sana moyoni:
Wakolosai 1:9-11 Kwa sababu hiyo sisi nasi, tangu siku ile tuliposikia, hatuachi kufanya maombi na dua kwa ajili yenu, ili mjazwe maarifa ya mapenzi yake katika hekima yote na ufahamu wa rohoni; mwenende kama ulivyo wajibu wenu kwa Bwana, mkimpendeza kabisa; mkizaa matunda kwa kila kazi njema, na kuzidi katika maarifa ya Mungu; mkiwezeshwa kwa uwezo wote, kwa kadiri ya nguvu ya utukufu wake, mpate kuwa na saburi ya kila namna na uvumilivu pamoja na furaha.
Tunapoendelea kutembea pamoja kwenye vipindi hivi kila siku, basi hayo ndiyo maombi yangu kwa ajili yako.
Hili ndilo Neno la Mungu safi na lenye afya kwa ajili yako leo.